Bashiru Ally Kakurwa (alizaliwa Wilaya ya Bukoba Vijijini, 1 Januari 1968[1]) ni mwanasiasa nchini Tanzania.
Alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi tarehe 31 Mei 2018.[2][3][4]
Kabla ya kuwa katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Bashiru alikuwa mhadhiri katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Tarehe 26 Februari 2021 aliteuliwa na rais John Pombe Magufuli kuwa katibu mkuu kiongozi [5], lakini tarehe 31 Machi 2021 aliteuliwa na rais mpya Mama Samia Suluhu Hassan kuwa mbunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania [6].
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search